Ijumaa , 26th Mei , 2017

Muigizaji Jacquline Wolper amekanusha vikali kuhusu suala la kuwahi kubadilisha dini kwa shinikizo la mapenzi na kwamba yote yaliyowahi kuonekana au kusikika huko nyuma ni mambo ya sanaa.

Jacqueline Wolper wakati alipodai kuwa muumini wa dini ya kiisilamu

Wolper amefunguka hayo na kudai kwamba yeye kama msanii kuna mambo anaweza kufanya ya kisanii lakini watazamaji wasijue kama ni sanaa lakini ukweli ni kwamba hajawahi kuhama ukristo na kwenda kwenye dini ya kiislamu.

"Sijawahi kubadilisha dini mimi, Sisi wasanii ndiyo tunajua tunafanyaga mimi mpaka watu wanaamini vitu kama kubadilisha dini. Ukweli wa dini yangu naujua mimi peke yangu lakini mengine yanayoonekana ni kazi ya sanaa" -Wolper alifunguka.

Akizungumzia suala la mapenzi Wolper amesema kwamba amekuwa na changamoto mbalimbali sana za kushindwa kudumu kwenye mahusiano kwa kuwa wanawake wenzake hupenda kumuingilia kwenye mahusiano yake kitu ambacho amekiita kipaji cha kukomeshwa.

"Mimi ni kama nina kipaji cha kukomeshwa kwenye mapenzi kwa sababu kipaji ninachokivumbua mimi wenzangu wanataka wapite hapo hapo ili kunikomoa. Ni kwamba nina kipaji cha kukomeshwa lakini huyo anayenikoa unakuta hajui mimi nimepambana vipi kumtengeneza mtu anipende" aliongeza Wolper.

Mtazame hapa akifungukia sakata lake