Ijumaa , 5th Mei , 2017

Zuwena Mohamed ' Shilole' anayetamba na hit ya 'hatutoi kiki' amefunguka na kudai kwamba haitaji kuolewa na mwanaume mwenye pesa kwani wengi wao hutumia mali zao kama fimbo ya kuwachapa na  kunyanyasia wanawake zao.

Shilole akiwa kikaangoni EATV

Akiwa Kikaangoni kwenye ukurasa wa Facebook wa EATV, Shilole amefunguka kuwa yupo tayari kuolewa lakini mpaka atakapo pata mwanaume atakayekidhi vigezo vyake huku akitaja pesa siyo kitu anachokitanguliza bali heshima, upole na ukarimu.

"Natamani sana kuolewa lakini mpaka nimpate mtu mwenye vigezo ninavyohitaji mimi, napenda mwanaume anayejali, atakayeniheshimu lakini awe pia anafanya kazi kama hafanyi kazi simtaki. Lakini pia wanaume wenye pesa siwataki maana tunawaona huko majumbani wanavyotumia kama fimbo kuwanyanyasa wake zao"- Shilole alifunguka.

Shilole hajaishia hapo ameendelea kufunguka kuhusu suala la muonekao "mimi siangalii sana muonekano kwani unaweza kutengenezwa lakini ukiwa mfupi mimi sitakukubali nahitaji mwanaume mrefu na mwenye heshima na anayejituma kwenye utafutaji"- aliongeza Shilole.