Alhamisi , 26th Sep , 2019

Mbunge wa Jimbo la Temeke Abdallah Mtolea, amesema hakumbuki fadhila zozote alizowahi kufanyiwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama chake cha zamani CUF, Maalim Seif na Mwenyekiti wake wa sasa, Prof. Ibrahim Lipumba.

Mtolea ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye kipindi cha #Kikaangoni kinachorushwa kila Jumatano kupitia kurasa za Facebook na Youtube ya East Africa TV, ambapo amesema hakumbuki chochote alichofanyiwa na viongozi hao, kwa sababu ameshaondoka upande huo.

"Kiukweli kwa sasa hivi siwezi kuzungumzia jambo ambalo liamuhusu Lipumba kwa sasa nimeshaondoka, mimi nilishamalizana na nimeshasahau, kwa sababu jinsi tunavyoishi CCM, huwezi kukumbuka nyuma siwezi nikajichosha na mambo ya watu wengine" amesema Mbunge Mtolea

"Kuhusu Maalim Seif sina chochote cha kumzungumzia, na wala sikumbuki chochote kuhusu yeye kama alininadi mimi kwenye kampeni zangu, na mtu akisema sina fadhila atakuwa amekosea." amesema Mtolea

Tazama mahojiano kamili hapo chini.