Jumatano , 16th Oct , 2019

Msanii wa muziki wa Injili nchini Joel Lwaga, amesema si jambo la ajabu kwa mtumishi wa Mungu, kunyoa aina yeyote ya nywele kwa kuwa kinachoangaliwa zaidi ni ujumbe ambao mtu huyo anautoa kutoka kwenye kinywa chake.

Joel Lwaga ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye kipindi cha Kikaangoni, kinachorushwa kwenye kurasa za Facebook na Youtube ya East AfriCA TV, kila siku ya Jumatano ambapo amedai yeye hajutii kunyoa mtindo wa nywele.

"Kwani nikinyoa hivi inamtesa nini mtu anayenifuatilia?,mafuta ya nywele ninayopaka siyajui jina ila bei yake hayazidi elfu 8" - amesema Joel Lwaga.

Aidha Msanii huyo amesema kuwa "napenda sana saa za mkononi, ila sijawahi kununua inayozidi shilingi laki mbili' ,Joel Lwaga.

Tazama mahojiano kamili hapo chini