Jumanne , 15th Mar , 2022

Msanii wa filamu Bongo @elizabethmichaelofficial 'Lulu' ameshea moja ya mipango yake ilikuwa ni kupata mtoto mapema katika umri wa miaka 22 au 23.

Picha ya Elizabeth Michael

Akimjibu shabiki kwenye Insta Story yake ambaye amemuuliza kwamba alipanga kupata mtoto akiwa na umri gani?

"Mipango yangu ya mwanzo kabisa nipate mapema kama nikiwa na miaka 22 au 23, baada ya kurudi kwenye kikao na halmashauri ya kichwa changu nikasogeza mpaka mwaka 2022, lakini Mungu kanibariki mwaka mmoja kabla ya mipango yangu".

Kwa sasa Elizabeth Michael ana miaka 26 na mtoto mmoja wa kiume.