Ijumaa , 26th Mei , 2017

Malkia wa filamu bongo, Jacqueline Wolper amefunguka na kukiri kwamba alishawahi kutoka kimapenzi na msanii Alikiba huku akidai ndiyo mahusiano pekee yaliweza kudumu kwa muda mrefu na namba moja kwa uzuri mpaka sasa.

Msanii Alikiba Kushoto, kulia ni Muigizaji Wolper

Wolper amebainisha hayo kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa mubashara kupitia ukurasa wa facebook EATV, baada ya kuulizwa swali lilomtaka aseme ni mahusiano yake gani aliyowahi kuwa nayo anaweza kuyapa nafasi ya kwanza kwa ubora mpaka hii leo.

“Katika wanaume wote niliowahi kuwa nao, mahusiano yangu na Ali Swalehe Kiba, 'Alikiba' ndiyo yalikuwa 'the best" - alisema Wolper.

Pamoja na hayo, Wolper amesema hawezi kukumbuka ameshatoka na wanaume wangapi mpaka muda huu kwa kile anachokidai kuwa anatatizo la kupoteza kumbukumbu (usahulifu).

Mtazame hapa chini Wolper akifunguka