Jumanne , 3rd Dec , 2019

Msanii wa filamu nchini, Esha Buheti, amesema kuwa ndani ya mkoba wake mara nyingi huwa anatembea na kiasi kidogo cha pesa, ambacho huwa anakitumia kwa ajili ya matumizi mbalimbali pindi anapokuwa kwenye mizunguko yake ya kila siku.

Msanii wa filamu nchini, Esha Buheti.

Esha Buheti ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye kipindi cha KIKAANGONI, kinachorushwa kwenye kurasa za Facebook na YouTube ya East Africa TV, wakati akijibu swali lililomtaka kutaja kiasi cha pesa ambacho huwa anatembea nacho na ndipo alipotoa kiasi cha Shilingi Elfu 89 na kusema ndicho alichonacho na kwamba pesa zake nyingi huwa anazihifadhi kwenye simu.

"Kama ningejua ungeniuliza kiasi cha pesa ninachotembea nacho, sijui ningekufanya nini wewe mtangazaji(Sangu Joseph), ila mimi natembea na Shilingi Elfu 89, japo ni kiasi kidogo sana kwa mwanamke ila mimi ndiyo nimekibeba" amesema Esha Buheti.

Aidha katika mahojiano hayo Esha Buheti, alitishia kuondoka ndani ya kipindi baada ya kuambiwa aigize akimteta Wema Sepetu, namna ambavyo kwa sasa amefulia.

Tazama mahojiano kamili hapo chini.