"Wanaume wembamba ndiyo ugonjwa wangu" - Asha Boko

Ijumaa , 8th Jan , 2021

Kila mtu huwa ana kitu chake anachokipenda au kukuzimia pale anapokuwa na mtu kwenye kwenye mahusiano au ndoa, sasa huyu hapa ni msanii wa filamu Asha Boko ambaye amefunguka kusema anawapenda sana wanaume wembamba pia ndiyo ugonjwa wake.

Asha Boko na mume wake Duwa Msafiri

Asha Boko amejibu hilo kupitia EATV & EA Radio Digital, baada ya mashabiki wengi wa mitandaoni kujaji umri na muonekano wa mume wake ambaye wameoana siku kadhaa zilizopita amesema kuwa,

"Mume wangu nipo naye miaka miwili iliyopita, ila ni wembamba wa reli na sio kusema kwamba ni mdogo halafu mimi wanaume wembamba ndiyo ugonjwa wangu, umri wangu au wake hauwahusu wajue tu ni mkubwa wala sio mtoto kwanza hata marehemu mume wangu wa kwanza kimwili chake kama huyu wa sasa" amesema Asha Boko 

Bonyeza hapa kutazama Interview kamili.