"Wanasema nioe kwanza, ndio niweze zungumza" Idris

Alhamisi , 1st Apr , 2021

Mchekeshaji maarufu Bongo Idris Sultan amevunja ukimya kwa kuwaambia wazazi kwamba kuna sehemu wanatakiwa kuhakiki vizuri hasa kwenye masuala ya ndoa kwa sababu watoto wao wanakutana na matatizo makubwa.

Mchekeshaji Idris Sultan

Idris Sultan amesema baadhi ya wazazi wanaogopa kuwaambia watoto wao kutoka kwenye ndoa kwa sababu ya maneno ya watu hali ya kuwa mtoto wao anakutana na matatizo kama kuteswa kimwili, msongo wa mawazo, majeraha au kisaikolojia.

"Ila wazazi kuna kasehemu flani inabidi mfanye 'review' ya kina, unamshauri mwanao abaki kwenye ndoa ambayo anateseka si kwa dunia bali anateswa na mwenza wake, kimwili ama kisaikolojia, ana msongo wa mawazo na hata majeraha mwilini, yote haya kisa wewe unaogopa maneno ya watu".

Aidha mchekeshaji huyo ameongeza kueleza kuwa  "Watu wanasema nioe kwanza ndio niweze kuzungumza, sasa nanyi pia tembeeni maeneo ya Jeshi yaliyoandikwa 'usipite tahadhari mabomu' Pia vuka barabara bila kucheki left na right, ugongwe kwanza ndio utuambie kuhusu barabara na usalama".

Zaidi tazama interview ya Mkalimani aliyezua gumzo mitandaoni.