Jumamosi , 24th Sep , 2016

Wananchi mbali mbali wa jiji la Dare es salaam wametoa maoni yao kuhusu kuanzishwa kwa EATV AWARDS kwa wasanii wa muziki na filamu kwa Afrika Mashariki.

Wakitoa maoni yao kwenye East Africa Television, baadhi ya wananchi wamesema hilo ni jambo jema kwenye tasnia ya sanaa, na kusema ni heshima kubwa kwa wasanii na kuwapa fursa ya kujitambua uwezo wao.

“Actualy mjue tuzo ni heshima, kwa hiyo cha kwanza msanii anapata heshima, cha pili inakuwa inampa nguvu ya yeye kujikubali na kuelewa kwamba mimi nafasi yangu iko sehemu gani, kwa sababu mpaka kufikia hatua ya kupewa tuzo ujue ni hatua kubwa sana", alisema Paul Pascal mkazi wa Dar es Salaam.

Naye kijana aliyejitambulisha kwa jila na K-Zo alisema ... “Mi nahisi kuja kwa tuzo mpya za East Africa zitasaidia sana kukuza mziki ukizingatia zinacombine wasanii wengi kutoka nchi mbali mbali ambazo zinatuzunguka, kwa hiyo zitachangia kunyanyua mziki kwa kiasi kikubwa sana, na pia zitasaidia wasanii wa nyumbani kupata conection kutoka sehemu tofau tofauti”,.

Kuhusu utaratibu wa kujisajili wananchi hao walisema wao kama mashabiki wameona ni mfumo mzuri kwani umeweka uwazi kwenye kila kitu, na kuwafanya wananchi wafahamu mchakato mzima unavyokuwa na kuepuka malalamiko.

“Kumekuwa na uwazi mwingi kiasi kwamba hata sisi wananchi wa kawaida tumekuwa tunajua nini kabisa kinaendelea, tunaona saa hizi wasanii wachukua form na wanajisajili pia, alafu hata namna ya kupigiwa kura ni tofauti kidogo, kwa sababu tuzo zilizopita mi nilikuwa sijui nani amechaguliwa, sikujua hata wasanii wanachaguliwa kwa style ipi”, alisema Paul Pascal ambaye ni mkazi wa Dar es slaam.

EATV AWARDS zinatarajiwa kufika kilele chake tarehe 10 Desemba 2016, ambapo ndio kutakuwa na sherehe za utoaji wa tuzo hizo.