Alhamisi , 25th Nov , 2021

Mr PKP Ommy Dimpoz 'is back' baada ya ukimya wa miezi 11, tegemea kazi yake mpya akishirikiana na fundi wa muziki Africa Fally Ipupa kutoka nchini Congo DR baada ya kushea picha yao wakiwa pamoja studio.

Ommy Dimpoz kulia, kushoto ni Fally Ipupa

Katika picha hiyo Ommy Dimpoz anasema "Haya viuno vyenu vitieni grisi mapema, Dimpoz X Fally".

Ommy Dimpoz anakuwa msanii wa pili kufanya kazi na Fally Ipupa baada ya Diamond alivyofanya hivyo mwaka 2019.