Jumatatu , 27th Mar , 2017

Mkali wa bongo fleva Barnaba Classic ambaye anatamba kwa kibao chake matata kinachopewa jina la 'Lonely' usiku wa kuamkia leo Jumatatu amelizwa vitu vilivyokuwa ndani ya gari lake na watu wasiojulikana.

Barnaba

Msanii huyo ameandika kwenye ukurasa wake wa instagramu kuwa ameibiwa begi dogo ambalo ndani yake kulikuwa na 'Laptop' mbili za aina ya 'Mac' moja Pro X Letina(Kompyuta mpakato), External mbili, faili lake lenye mikataba mbalimbali pamoja na hati ya kusafiria 'Passport'.

"Naomba sana sana waungwana kama kuna mtu yotote atabaini au kujua vilipo au hata kupelekewa basi naomba wasamalia wema mnirudishie au kuniletea  napatikana kwa 'No 0743505010' Mungu awabariki  naamini aliyenavyo hajaiba bali amepitiwa katika njia ya kutafuta riziki nami kwa jina la Mungu nitamsamehe na nimesamehe ila kama ana rohoo nzuri na ameguswa basi naomba waungwana mnipigie hata kama umeokota". Ameandika Barnaba