Jumanne , 23rd Mei , 2017

Wakali wawili katika anga la bongo fleva Alikiba na Mr Blue ambao wameendelea kufanya vyema kwa muda mrefu, mwaka jana walikutana tena kwenye ngoma mbili, moja ikiwa ile ya Abby Skillz 'Averina' na ile ya Mr Blue 'Mboga saba'

Alikiba na Mr. Blue

Wimbo uliowakutanisha Mr Blue na Alikiba 'Mboga saba' ni wimbo ambao ulikuwa na mafanikio makubwa sana na kutazamwa na watu wengi kwenye mitandao ya jamii hasa 'You tube' lakini usichokijua juu ya ngoma hii ni kwamba video ya wimbo huu ilifanyika kipindi cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan ambapo ilimbidi Mr. Blue afungulie ili aweze kufanya baadhi ya mambo katika video hiyo kama kula mihogo ya pale 'Coco beach' Dar es Salaam na kunywa maji ya dafu.

Lakini kwa upande wa Alikiba yeye aligoma kabisa kutengua swaumu yake na ndiyo maana katika video ile alikuwa amevaa vazi moja tu mwanzo wa video mpaka mwisho wa video ile ya mboga saba. 

Jambo la mwisho ambalo wengi hawafahamu ni kuwa zile sauti za kike zinazosikika kwenye ngoma ile ni sauti za Maua Sama.