Jumatano , 22nd Mar , 2017

Msanii Cyril Kamikaze ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake mpya wa 'Sinunui stress' amesema siyo kweli kwamba muziki unakosa 'promo' pindi yanapotokea masuala makubwa ya kitaifa kwa kuwa kila jambo linakuwa na wadau wake

Kamikaze

Hayo yamekuja kutokana na baadhi ya wasanii kulalamika wanasiasa wamekuwa gumzo kubwa kipindi hiki jambo ambalo linawafanya wanashindwa hata kutambulisha kazi zao mpya kwa hofu zilizowajaa kutopewa muda na mashabiki zao kuzisikiliza.

“Siku zote muziki umekuwa na nafasi yake, inapotokea suala kubwa la kitaifa na kupata 'pressure' ya juu,naamini  bado wapenzi wa muziki watapata nafasi ya kusikiliza wanachokipenda kwa sababu kuna muda unakuwa na mzuka. Hivyo utafanya yote lakini utarudi tu kusikiliza muziki". Alisema Cyril

Kwa upande mwingine msanii huyo amewataka mashabiki zake wamshauri pale anapokosea ili azidi kufanya vizuri nasio kum-'diss' kwa kumwambia aache aina ya muziki anaoufanya kwa kuwa hatowasikiliza.