Ijumaa , 5th Mar , 2021

Kuelekea siku ya wanawake duniani, msanii Harmonize ametoa wosia kwa watoto wote wa kike ambapo amewaambia  wawe na maamuzi sahihi kwa wanachotaka kufanya kwenye maisha kwa sababu hakuna kitu kipya kwenye dunia.

Msanii Harmonize akiwa na mtoto wake wa kike Zulekha

Akizungumzia hilo kupitia kamera ya EATV & EA Radio Digital, Harmonize amesema akiona mtoto wa kike anakosea basi anahisi kama mwanae Zulekha ndiyo kakosea hivyo amewaomba wafanye vitu kwa wakati sahihi.

"Mtoto wa kike yeyote ambaye ananitazama sasa hivi anatakiwa ajue kwamba yeye ndio ana maamuzi ya kuchagua kutaka kuwa nani lakini hakuna kitu kipya kwenye hii dunia bibi yako, mama, dada na shangazi vyote walishafanya hivyo ni bora kuwa makini na kufanya vitu kwa wakati sahihi" amesema Harmonize

Zaidi mtazame hapa chini kwenye video.