"Uchebe sio domo zege" - Masha Lovie

Jumanne , 13th Oct , 2020

Mwanamitandao na mwalimu wa 'video vixen' Masha Lovie amekanusha madai ya kumtafutia mpenzi mpya mfanyabiashara Uchebe kwa kusema mwanaume huyo sio domo zege kwani anaweza kutafuta wanawake bila hata ya kutafutiwa.

Masha Lovie upande wa kulia,kati ni Uchebe akiwa mpenzi wake mpya Agness

Masha Lovie 'Don Dada' amejibu hayo baada ya kuonekana akiwa karibu na mpenzi huyo wa Uchebe aitwaye Agness, na kusambaa kwa taarifa mitandaoni kwamba yeye ndiyo amesababisha wawili hao kuwa pamoja.

"Uchebe ni mshkaji wangu tangu yupo na Shilole kwanini wanasema kwamba nimempa mwanamke, mahusiano yake mapya na mtu wake hata hayanihusu, nilivyonunua gari mtu wa kwanza kumwita ni Uchebe ili kuliangalia na kunisadidi kwenye mambo ya usajili, TRA na bima

"Siku alivyokuja kuangalia gari yangu ndiyo akaja na huyo mwanamke wake ndipo nilipomuona kwa mara ya kwanza, wasiseme kwamba huyo mwanamke ndiyo nimempa kwanza Uchebe sio domo zege anatafuta mwenyewe" ameongeza