Uchebe atoa kauli ya kibabe kwa mwanamke wake mpya

Ijumaa , 13th Nov , 2020

Aliyekuwa mume wa msanii Shilole, mfanyabiashara Uchebe amejibu mapigo kwa wanaoleta maneno kuhusu mpenzi wake mpya aitwaye Official Agness, kwa kusema sasa hivi yeye sio mume wa mtu na hayupo kwenye ndoa hivyo anaweza kuchukua mwanamke yeyote anayemtaka.

Picha ya pamoja Uchebe akiwa na mpenzi wake mpya Official Agness

Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio, Uchebe amesema kila mtu aangalie maisha yake na watu wasimjaji sana kwani hata yeye ana 'protocal' binafsi za maisha yake.

"Sipo kwenye ndoa na sasa hivi mimi sio mume wa mtu, nina uwezo wa kutoka na yeyote na kufanya chochote kama mwanaume, na mwanaume lazima amfuate mwanamke ili kujua anataka nini haijalishi awe muislam au muikristo" amesema Uchebe

Aidha ameongeza kusema "Maisha yapo tofauti wasijaji sana kuhusu mimi waangalie maisha yao yanaenda vipi, mimi pia nina protocal zangu kwa mwanamke kwanza awe anafanya ibada na asinywe pombe maana siwezi kukaa na mwanamke mlevi kwangu".