Tunda Man afunguka kuacha muziki kupitia Alikiba

Jumamosi , 12th Sep , 2020

Hivi unaikumbuka ile ngoma ya Msambinungwa ya Tunda Man na Alikiba iliyotoka mwaka 2014, kama ni ndiyo basi tarajia ladha ya wimbo mwingine kutoka kwao ambapo msanii Tunda Man amesema huenda ndiyo kazi yake ya mwisho kuacha muziki.

Wasanii wa BongoFleva kulia ni Alikiba, kushoto Tunda Man

Akifunguka kupitia EATV & EA Radio Digital, Tunda Man amesema

"Nimeshafanya ngoma na Alikiba ilifanya vizuri dunia nzima, pia tumefanya kazi nyingine kwa producer Maneck ambayo ni kubwa sana kiasi kwamba naona nikiichia hivi karibuni itaweza kuwa ndiyo kazi yangu ya mwisho kwenye muziki, au unaweza kusema naacha muziki kabisa maana ni ngoma kubwa sana".