Tommy Flavour afunguka kuhusu kumchora Tattoo Lyyn

Jumamosi , 14th Nov , 2020

Msanii wa Kings Music Records Tommy Flavour, amesema tattoo zilizopo mwilini mwake ni za muda mrefu na wala hajawahi kuchora tattoo yenye jina au sura ya mpenzi wake Official Lyyn.

Msanii Tommy Flavour na mrembo Official Lyyn

Tommy Flavour amesema hatarajii kuchora tattoo ya mpenzi wake huyo kwa sababu hataki kujutia baadaye pia haamini kwamba kumchora mtu ndiyo atakuwa ameonyesha upendo kwake. 

"Sijawahi kuchora tattoo yenye jina lake wala sura yake na hata yeye hajanichora, tattoo ambazo nipo nazo ni za muda mrefu japo kuchora ni maamuzi yako mwenyewe, unaweza ukachora halafu baadaye ukajuta na mimi sitaki kufikia kwenye hali hiyo, sisemi hivi kama nitaachana naye au kuna lolote baya litatokea ila siamini kama nikifanya hivyo ndiyo nitakuwa naonyesha mapenzi kwake" ameeleza Tommy Flavour 

Zaidi mtazame hapa chini kwenye video.