Alhamisi , 30th Dec , 2021

Muigizaji Dwayne Johnson maarufu kama the “The Rock” amekataa ombi la kurejea kuigiza muendelezo wa filamu ya Fast & Furious sehemu ya 10.

Picha ya Vin Diesel kushoto kulia ni The Rock

Mwezi Novemba mwaka huu muigizaji Mark Sinclair “Vin Diesel” kupitia ukurasa wake wa instagram alimuomba The Rock arudi kumalizia sehemu ya mwisho ya Fast & Farious kwa ajili ya mashabiki wao na kutimiza ahadi yao kwa marehemu Paul Walker.

The Rock katika interview yake na CNN iliyochapishwa siku ya jana amekataa ombi la Vin Diesel kurejea katika Fast & Farious na kumkosoa kwa kitendo chake cha kuongolea suala hilo katika mitandao ya kijamii kwa kuwahusisha watoto na marehemu Paul Walker.

Nilishangazwa sana na post ile ya Vin Diesel, mwezi wa sita mwaka huu niliongea nae faragha na kumwambia sitaweza kuigiza tena filamu hiyo ila nitatoa ushirikiano wangu katika kuandaa filamu hiyo ili kuhakikisha inafanikiwa na hata washirki wengine wote niliongea nao na walinielewa.” Majibu ya The Rock

The Rock ameweka wazi msimamo wake hatarudi tena katika Fast & Furious na anawatakia kila kheri katika muendelezo wa filamu hiyo.