Jumanne , 24th Mei , 2022

Msanii Joseph Mbilinyi Mr II Sugu amezungumzia suala la afya ya Professor Jay kwa kusema anaendelea vizuri na kupambania afya yake.

Picha ya pamoja ya Prof Jay na Mr II Sugu

Kupitia Planet Bongo ya East Africa Radio Sugu anasema 

"Tupo in-touch kama familia na anaendelea vizuri, kitu kizuri ni kwamba yeye mwenyewe (Prof Jay) yupo kwenye spirit ya kupambana, ukishakuwa kwenye spirit ya kupambana hata mwili wenyewe unajiandaa kupokea matibabu".

Planet Bongo ni kila siku ya Jumatatu mpaka Ijumaa kuanzia saa 7:00 mchana mpaka 10:00 jioni.