Stamina afunguka Rais Magufuli kupenda wimbo wake

Alhamisi , 18th Mar , 2021

Msanii wa HipHop hapa nchini Stamina Shorwebwenzi amesema atamkumbuka Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kila kitu hasa kufanya mambo mengi na makubwa ndani ya muda mfupi ya uongozi wake.

Rais Dkt John Pombe Magufuli, kushoto ni msanii Stamina

Stamina Shorwebwenzi ameendelea kusema ataomboleza kwa kukumbuka kwa mema yake yote kama kiongozi na wala hatamkumbuka kwa mabaya.

Aidha msanii huyo amezungumzia suala la Rais Magufuli kuupenda wimbo wake wa baba aliomshirikisha Prof Jay ambapo amesema, 

"Kauli kutoka kwa Rais inakuwa sheria kwa hiyo kumfanya Rais aupende wimbo wako sio kitu kidogo ila mpaka nimekuwa mimi ni kitu ambacho ni cha heshima na kimenihimiza sana, nilifurahi na kilinipa nguvu" 

"Kwangu mimi haikuwa kitu cha ajabu kwa sababu hata wimbo wangu wa asiwaze alikuwa anaupenda pia tulivyokuwa kwenye kampeni aliweza kutuambia, niliona vitu ninavyovifanya Rais anavipenda na alikuwa anakubali aina ya muziki wangu" ameongeza

Zaidi tazama hapa chini akizungumzia hilo.