"Sitamani Ubunge nataka kuwa Rais wa Nchi" - Kala

Jumatatu , 15th Feb , 2021

Msanii wa HipHop Kala Jeremiah amesema akiingia kwenye kwenye siasa hatamani kuwa Mbunge bali anataka kuwa Rais wa Taifa hili kwa sababu anaijua nchi nje ndani.

Msanii wa HipHop Kala Jeremiah

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital Kala Jeremiah amesema akiwa Rais ataleta mabadiliko ambayo anaona yatafaa pia tayari ana wimbo unaoitwa ningekuwa Rais aliozungumzia masuala mengi juu ya uongozi.

"Mwaka 2010, 2015 na 2020 nimeombwa sana kugombea Ubunge mpaka vijana wananifuata nyumbani kutaka kunichukulia fomu lakini utayari ninanukuwa sina, nitakapokuwa ninaingia kwenye siasa sitamani kuwa Mbunge nitaingia kwa sababu nataka kuwa Rais wa Nchi, nitaleta mabadiliko ninayoyaona mimi na naijua nchi nje ndani" ameeleza Kala Jeremiah 

Zaidi mtazame hapa chini akizungumzia kwa urefu zaidi.