"Sio rahisi kuwa na wake watatu au wanne" - Mwaka

Ijumaa , 9th Oct , 2020

Tabibu wa tiba za asili, mimea na matunda Dkt JJ Mwaka amesema huwa anajiuliza watu wanaposema kwamba wanatapa ushawishi kupitia yeyewa kuoa wake zaidi ya mmoja kwani jambo hilo sio rahisi kama wanavyofikiria.

Dkt JJ Mwaka kwenye kipindi cha SalamaNa ya East Africa TV

Akipiga stori kwenye kipindi cha SalamaNa ya East Africa TV ambayo inaruka kila siku ya Alhamisi kuanzia 3:00 usiku Dr Mwaka ameeleza kuwa "Mimi naona watu wengi wanafikiria kirahisi sana kuoa wake watatu au wanne, wengi nikipita mtaani wananiambia mimi ni 'role model' wao sasa najiuliza nawahamasisha kwa kipi

Aidha ameongeza Dkt Mwaka ameongeza kusema "Nina watoto 7, wawili wa mke wa kwanza, baadaye nikaoa mke wa pili nikazaa naye watoto wawili lakini nikamuacha, nikaoa tena mke mwingine nikazaa naye watoto wawili, halafu nikaoa mke wa tatu nikazaa naye wengine wawili lakini mmoja alifariki"