Jumatatu , 15th Mar , 2021

Ni 'headlines' za msanii na mkali wa kucheza Msami Baby ambaye amejitokeza na kusema hamjui Kajala Masanja ndio nani baada ya kuwa na uvumi mitandaoni unasemekana aliwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na msanii huyo wa filamu.

Picha ya Msami Baby kulia na Kajala kushoto

Akijibu hilo kupitia EATV & EA Radio Digital,  Msami Baby amesema kuwa "Mimi kiukweli nimekuwa naulizwa sana hilo katika siku za hivi karibuni lakini huwezi amini mimi simjui kabisa Kajala ni nani

"Najaribu kuvuta picha watu wananiambia kuhusu yeye lakini simjui ni nani mpaka najiuliza kwamba kuna watu wamenifananisha na mtu, mimi simjui" ameongeza

Zaidi mtazame hapa kwenye video akizungumzia hilo.