Sababu za Mabeste kufanya muziki wa Injili

Alhamisi , 24th Sep , 2020

Msanii wa HipHop Mabeste amesema ameamua kumshukuru Mungu kwa kuachia nyimbo ya injili ambayo ni kwa ajili ya kumtukuza  na shukurani kwa mahali ambapo amemfikisha na alipomtoa.

Msanii wa Mabeste

Akiongea na eNewz ya East Africa TV Mabeste amesema wimbo wake unayofuata ni kwa ajili ya Mungu kutokana na kujiona anabadilika kuwa mpya kila siku.

Nyimbo ninayotoa ni Gospel kutokana na Mungu aliponitoa na apa nilipo niko mpya zaidi ya jana kwenye kila kitu nazidi kujipenda zaidi na kujielewa zaidi na nazidi kumshukuru Mungu, hii ni Mabeste katika Sanaa yake nimeshawaburudisha sana katika aina ya muziki wa bongo fleva sasa nawaburudisha katika injili hii ni kwaajili ya kujipenda” - amesema Mabeste 

Zaidi tazama hapa chini kwenye video.