Rose Ndauka adaiwa mapacha wawili na mumewe

Jumatano , 6th Jan , 2021

Mume wa msanii wa filamu Rose Ndauka, Haffiyy Mkongwa amesema bado anamdai mkewe huyo watoto wengine wawili tena atafurahi kama ikiwezekana wawe mapacha ili waweze kumaliza kwa haraka.

Rose Ndauka, Mumewe Haffiyy na mtoto wao

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, mumewe huyo amesema kwa sasa tayari wamepata mtoto mmoja na Rose Ndauka hivyo anasubiria mpaka atakapofikisha miaka miwili ndiyo wataongeza wengine.

"Tunashauriwa na Serikali na vyombo vingine mbalimbali vya kiafya kwamba mtoto afikishe angalau miaka miwili ndiyo muweze kupata mwingine ila binafsi nitangoja mpaka akue kabisa na kujitambua, nataka watoto wengine wawili na ikiwezekana wawe mapacha ili tuweze kumaliza kwa haraka" amesema Haffiyy Mkongwa

Haffiyy Mkongwa na Rose Ndauka wamefahamiana kipindi cha miaka mitano iliyopita na wamefunga ndoa mwaka 2020 na tayari wamebahatika kupata mtoto mmoja wa kiume aitwaye Prince Haleem.

Bonyeza hapa kutazama Interview kamili