Alhamisi , 23rd Dec , 2021

Roma Mkatoliki ametoa ya moyoni kwa kinachoendelea mitandaoni kwa baadhi ya watu kumsema Lulu Diva kutojenga nyumbani kwao Muheza Tanga wakati yanafanyika mazishi ya mama yake mzazi.

Picha ya msanii Roma Mkatoliki

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Roma ameandika kwamba 

"Tunapofiwa/kupata matatizo yanayopelekea mkafika nyumbani kwetu, please fikeni na mshiriki kwenye matatizo hayo tu mkimaliza mrudi makwenu salama".

"Haya mambo ya kwanini hujajenga kwenu, sijui muoneni ana-ball tu town ila kwao hajajenga hayawahusu, town kila mtu ana mipango yake bana".