Rasmi Lulu afunga ndoa na Majizzo leo

Jumanne , 16th Feb , 2021

Ni 'Headlines'  za staa wa filamu hapa nchini Tanzania Elizabeth Michael maarufu kama Lulu ambaye rasmi kabisa siku ya leo Februari 16,2021 amefunga pingu za maisha na mpenzi wake wa siku nyingi Francis Ciza 'Majizzo'.

Elizabeth Michael na Majizzo wakiwa wanafunga ndoa leo

Kupitia picha ambazo zimepostiwa mitandaoni zimeonesha wawili hao wakila kiapo cha kufunga ndoa hiyo ambayo imefanyika  katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Gasper, Mbezi Beach Jijini Dar es Saalm.

Mahusiano ya Elizabeth Michael Lulu na Majizzo ni ya muda mrefu na walikuwa wote kwenye kipindi ambacho Lulu alikuwa na kesi ya kuua bila kukusudia na kufikia Septemba 30, 2018 Majizzo alimvalisha pete ya uchumba Lulu.