Picha ya msanii Rihanna
Rihanna alichaguliwa kuwa balozi wa visiwa vya Barbados mwaka 2018, leo ameingia katika list ya mashujaa wa taifa hilo jipya Duniani likijitegemea kama Jamhuri kwa mara ya kwanza.
Dame Sandra Mason amechaguliwa kuwa rais wa kwanza wa Barbados amemtangaza Rihanna kuwa shujaa wa taifa hilo kwa mchango wake mkubwa katika kulitangaza taifa hilo kupitia kazi zake za sanaa na amefanya watu wengi kuvijua visiwa vya Barbados.