Prof Jay afunguka alivyompeleka mchepuko nyumbani

Jumanne , 16th Feb , 2021

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mikumi na msanii wa HipHop Joseph Haule 'Prof Jay' amefunguka kusema aliwahi kumpeleka mchepuko nyumbani kwa mkewe Grace Mgonjo wakati ambapo walikuwa wamegombana.

Picha ya pamoja Prof Jay na mkewe Grace Mgonjo

Prof Jay amesema mapenzi yao yamepitia mambo mengi na wakati tukio hilo linatokea walikuwa hawana mahusiano mazuri pia alivyompeleka mwanamke mwingine nyumbani kwa mkewe, alimuona mkewe huyo akitetemeka kama simu.

"Mahusiano yetu yamepitia kushuka na kupanda hadi tukaachana yeye akawa na mahusiano na mimi nikawa na mahusiano mengine, sasa kwa bahati mbaya nikambebea yule niliyekuwa naye kwenye mahusiano na nikaenda naye kwa mke wangu, kitu hicho kilimuumiza kuliko vitu vyake vingine, nilimuona akitetemeka kama simu" amesema Prof Jay 

Zaidi tazama hapa chini kwenye video.