Alhamisi , 15th Oct , 2020

Mtayarishaji wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini Tanzaniza Producer S2Kizzy ameeleza kuwa amevamiwa studio kwake ya 'pluto world' iliyopo Sinza Lion, kisha kupigwa na kufanyiwa uharibifu wa vifaa vyake na watu wanaodai wao ni walinzi shirikishi.

Producer S2Kizzy akiwa kwenye shughuli zake

S2Kizzy amefahamisha hilo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram ambapo ameandika kuwa

"Nimevamiwa studio, kupigwa na kufanyiwa uharibufu wa studio nzima, kuvunjiwa vifaa vya   na vitu vya studio na hawa wanaodai wao ni 'security' na ulinzi shirikishi, studio kulikuwa na watu ambao walipigwa kama wezi wanawake walizalilishwa ikiwemo kuvuliwa nguo, kupigwa na kufanyiwa vitendo vya kinyama

"Nimesikitisha na nimekatishwa sana tamaa mimi kama kijana ambaye natafuta riziki, kazi zeu tunakesha na tunahangaika lakini mwisho wa siku tunavunjwa sana moyo na vitu ambavyo havina hivi ili wala lile" ameongeza 

Tumejaribu kumtafuta Producer huyo ili atolee ufafanuzi zaidi juu ya chanzo cha tukio hilo ila kwa bahati mbaya hakuweza kushika simu yake.