Official Nai kuachana na Moni Centrozone kisa Fred

Jumatano , 14th Oct , 2020

Video Vixen Official Nai amefunguka kusema amechana na mpenzi wake Moni Centrozone baada ya kuhisiwa kuwa ana mahusiano na mfanyabishara wa mavazi Fred pia wamegombana kwa sababu ya kesi za wanawake ambazo zilikithiri kwenye mahusiano yao.

Msanii Moni Centrozone na Official Nai

Official Nai amesema Moni Centrozone alikuwa anahisi hivyo tangu kipindi cha nyuma kabla ya kutamka hadharani siku za hivi karibuni ila hakuna ukweli wowote kuhusiana na madai hayo.

"Sijawahi kutoka na Fred japo ikitokea naweza kuwa naye ila kwa sasa sijawaza na sijafikiria, kwanza mimi na yeye tumeongea  mara moja tu tangu suala hili kuzungumziwa zaidi mitandaoni anaona kama nimefanya kiki, Moni alinza kuhisi hivyo muda mrefu na tumeachana mwezi wa tatu au wanne, yeye ndiyo aliumiza sana moyo wangu alikuwa anatoka na watu wangu wa karibu kama wadogo zangu" ameeleza Official Nai 

Ziadi tazama hapa chini kwenye video.