Nandy ahojiwa na Koffi Olomide

Jumapili , 14th Feb , 2021

Imekuwa kawaida wasanii wa Bongofleva kuachia video na Audio kwa pamoja, lakini kwa Nandy imekuwa tofauti kwenye collabo yake na Koffi Olomide baada ya kutanguliza audio, jambo ambalo limefanya mashabiki wake wasubiri video kwa hamu.

Koffi Olomide na Nandy

Nandy pia ameonesha kutambua kiu ya mashabiki wake kwenye kuisubiri video hiyo ya #Leoleo na kupitia page yake ya Instagram amekutana na Koffi ambapo amepost video akidokeza kuwa maongezi yake na Koffi ilikuwa ni juu ya kuachia video hiyo. Hata hivyo bado hajaweka wazi ni lini ataiachia.

''Hapa anasema mbona siachii VIDEO? Nikamwambia tulia MOPAO watu hawana haraka wanaruka rumba'', ujumbe alioandika Nandy kwenye video fupi aliyopost akiwa na Koffi.

Audio ya Collabo hiyo imepandishwa YouTube siku ya Feb 11, 2021 na mpaka sasa imetazamwa zaidi ya mara laki tano.