"Naimba kuliko wasanii wote wa Bongo" - Ebitoke 

Jumatatu , 16th Nov , 2020

Mchekeshaji Ebitoke amesema sasa hivi anataka afahamike kama mwanamuziki kwa sababu ameingia rasmi katika tasnia hiyo na amefika mbali zaidi kwa kusema hakuna msanii yeyote anayemuweza kwa kuimba katika kiwanda cha BongoFleva.

Mchekeshaji, mwanamuziki na muigizaji Ebitoke

Akizunguzmia hilo wakati anapiga stori na EATV & EA Radio Digital, Ebitoke amesema kuwa ameingia kwenye muziki kwa sababu anaupenda na ana uwezo wa kuimba na wala hajafuata mkumbo kama wasanii wengine walivyofanya.

"Nataka nitambulike kama mwanamuziki na muigizaji, nimeingia kwenye muziki kwa sababu naupenda na nimeona nina uwezo wa kuimba tena naimba kuliko msanii yeyote wa hapa Bongo na hakuna anayenifikia, najua ni kawaida mashabiki kuongea na wapo watakaonipinga na wengine watanisapoti" amesema Ebitoke 

Zaidi tazama hapa chini kwenye video.