"Naenda msikiti, siwezi kupangiwa" - Muna

Jumatatu , 14th Sep , 2020

Kupitia EATV & EA Radio Digital, Mtumishi wa Mungu Muna Love ameeleza kuwa hawezi kupangiwa kwenye imani na kuna wakati anaenda hadi msikitini kwa sababu mama yake alikuwa muislam.

Mtumishi wa Mungu Muna Love

Muna Love amesema ameamua kuishi kwenye maisha yake binafsi, hataki kupangiwa kitu chochote kwenye upande wa kumtangaza Mungu kwani waislam na waikristo wote sawa na nia yake ni kufikisha ujumbe.

"Sasa hivi naishi maisha yangu binafsi na maisha ya mtandao, pia nina mapatano yangu na Mungu ambayo hakuna mtu anayejua nitafanya kitu ambacho sijali binaadam atasema nini najua simkosei Mungu, mimi nipo kwa ajili ya kumtangaza,  kuna wakati naenda hadi msikitini kwa sababu hata mama yangu alikuwa muislam kwa hiyo siwezi kupangiwa kwenye imani, naamini wote tupo sawa" ameeleza Muna Love