Jumanne , 21st Dec , 2021

Mwili wa Mama mzazi wa msanii wa Bongofleva Lulu Diva tayari umezikwa nyumbani kwao Mafele Muheza mkoani Tanga, leo mchana baada ya kufariki dunia siku ya juzi Jijini Dar es salaam.

Mwili wa mama Lulu Diva ukipumzishwa kwenye nyumba yake ya milele

Mbunge wa Muheza Mjini Hamisi Mwinjuma Mwana Fa, Irene Uwoya, Whozu, Petitman Wakuache, Aristotee, Alice Kela  ni baadhi ya mastaa waliojitokeza kwenye mazishi ya mama wa Lulu Diva.