Mwarabu afunguka kuwa mlinzi wa Baba wa Rihanna

Ijumaa , 9th Oct , 2020

Moja kati ya tukio lililo-trend wiki hii ni 'bodyguard' maarufu wa wasanii Mwarabu Fighter kupiga picha na baba mzazi wa msanii Rihanna Ronald Fenty ambaye amekuja kutembea hapa nchini Tanzania.

kulia ni Mwarabu Fighter na baba wa Rihanna Ronald Fenty, kushoto ni msanii Alikiba

Inasemekana Mwarabu Fighter amepata dili la kumlinda baba huyo kipindi hichi ambacho yupo hapa nchini, sasa EATV & EA Radio Digital imempata mlinzi huyo ili kuzungumzia suala hilo ambapo amesema,

"Wale ni wageni tu, walikuja sehemu ambayo nilikuwepo ila hakuna jambo lolote,  walivyoona mishe zangu wakajua ninachokifanya maana kuna mteja wangu nilikuwa namlinda, kwa hiyo wakasogea kwangu wakawa wananiuliza maswali na tukabadilishana baadhi ya vitu kwa nia ya kibiashara zaidi, yote yanatokea ni mipango ya Mungu

Akizungumzia kufanya kazi na msanii Alikiba baada ya kuonekana kwenye mchezo wa SamaKiba 'Foundation' Mwarabu Fighter amesema  "Mimi nilisapoti SamaKiba kwa sababu ni kitu kikubwa wanachokifanya kwenye jamii hadi nikapiga naye picha ila sikupewa kazi ya kumlinda".

Aidha amesema sasa hivi ana vijana ambao anawafundisha kuhusu kazi ya kuwalinda wasanii ambapo kama msanii atahitaji kufanya nao kazi atawatoa kwa makubaliano binafsi.