Jumanne , 17th Jan , 2017

Rapa Fid Q amefunguka na kusema kuwa watu hawatakiwi kutishwa na msanii mwenye followers wengi kwenye mitandao ya kijamii wakidhani kuwa mtu huyo ndiyo maarufu sana au ndiyo kusema anakuwa na biashara sana kwenye soko la muziki.

Fid Q

Fid Q aliyasema hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo na kusema wapo baadhi ya wasanii ambao hawana watu wengi kwenye mitandao ya kijamii lakini ni wasanii wakubwa na wanaweza kufanya show zao wenyewe na wakajaza na makampuni makubwa yakawekeza pesa zao.

"Views za Youtube hazi'define' muziki kufika kwa watu, nina ushahidi wa muziki ambao una views nyingi youtube lakini watu hawaujui, Chameleone anaweza kufanya event hapa Tanzania na ikawa na sponsors, ikajaza watu mpaka sponsors wakaweka hela zao na hatokei hapa Bongo, sasa jiulize kwanini huyu ana followers wachache kwenye mitandao ya kijamii au ana views chache youtube lakini ana soko kubwa. Kuna watu ni maarufu mitandaoni lakini hawajulikani Mpitimbi hapo au Nanjirinji hakuna mtu anawajua lakini ukienda kucheki followers Instgram utakimbia" alisisitiza Fid Q 

Kutokana na hilo Fid Q anawataka watu kutodanganyika na maisha ya social networks akisema kuwa kuna maisha yenye uhalisia nje ya mitandao ya kijamii 

"Kuna wasanii wengine wana followers wengi lakini wakifanya show wanachezea za uso, sasa hao followers wanaishi wapi? Ina maana followers wengi ni feki? Hata kama wakiwa real wengi hawa exist katika real life, sababu mtu kama una followers milioni mbili unafanya event masaa haijazi hao followers wako wako wapi?  Alimaliza Fid Q