Mrembo muendesha bajaji aibua mapya "Wananiogopa"

Jumatatu , 30th Nov , 2020

Kutana na Happy Mushi maarufu kama 'dada bajaji' ambaye ni mama wa watoto wawili amefunguka kusema watu walikuwa wanamugopa na kumshangaa kwa sababu ya kazi aliyokuwa anaifanya kutokana na jinsia yake.

Happy Mushi akiwa kwenye bajaji yake

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, Dada Bajaji amesema ana muda wa mwaka mmoja tangu aanze kazi hiyo ya udereva na ndoto zake ni kumilikia bajaji yake mwenyewe na kusaidia familia yake.

"Kazi ya bajaji niliona itaniingizia kipato na kukidhi mahitaji yangu ndiyo maana nikaingia, kuna mtu nilikuwa namlipa ili kunifundisha, mwanzo walikuwa wananiogopa walidhani sitakuwa serious, kwa sasa mwanaume ambaye atataka anioe aniweke ndani simtaki atakuwa anaharibu kipaji changu cha kutafuta pesa" ameeleza Happy Mushi 

"Abiria wangu wakipanda hii bajaji ni maswali mwanzo mwisho na huwa nawajibu, sishangai watu wanavyonishangaa kwa sababu kwetu Tanzania inajulikana kazi ya bajaji ni ya wanaume ila nataka niwatoe mshangao wao sasa hivi wameanza kunizoea" ameongeza 

Maongezi zaidi tazama hapa chini kwenye video.