Mpenzi wa Vanessa Mdee aanza kujifunza Kiswahili

Jumatatu , 14th Sep , 2020

Mpenzi wa msanii Vanessa Mdee Rotimi ameonekana akijifunza kuongea lugha ya Kiswahili ambapo alikuwa anafundishwa baadhi ya maneno na mpenzi wake huyo.

Vanessa Mdee na mpenzi wake Rotimi

Rotimi ameonekana akifundishwa kutamka maneno hayo kupitia Insta Story ya Vanessa Mdee ambapo alikuwa anamwambia ataje maneno ya Kiswahili kama yafuatayo.

"Ahh Mama yangu, jamaani kabisa polee " amesema Mpenzi wa Vanessa Mdee, Rotimi 

Wawili hao wanakaribia kumaliza mwaka sasa tangu walipoanza mahusiano yao mwaka 2019, ambapo Vanessa Mdee alikuwa ametoka kuachana na msanii wa RnB Juma Jux.