Monalisa aanza na mikwara hii Simba Queen

Jumatano , 3rd Mar , 2021

Mara baada ya kutambulishwa kuwa msemaji wa klabu ya Simba Queen msanii wa filamu na shabiki wa klabu hiyo Yvonne Cherrie 'Monalisa' amewataka mashabiki wamchagulie jina la kazi.

Muigizaji Monalisa akitambulishwa na Fatema Dewji kuwa msemaji wa Simba Queens

Akieleza hilo kupitia post yake ya Instagram Monalisa ameandika kuwa "Mimi ni Simba jike, natamani mjue furaha yangu, Ahsante Mungu, wanasimba wote na mwisho ahsante kwa mama mlezi wa Simba Queens Fatema Dewji kwa kunikabidhi kijiti cha kuisemea timu yangu pendwa ya Simba Queens Tanzania"

"Sasa ni muda wa kazi na muda wa kuionesha dunia ukubwa wa Simba, huko mlipo furahini na mfurahi haswa mwisho naomba kutoa tangazo rasmi ya kwamba kila binti au mwanamke nchi hii ni shabiki wa Simba Queens, nichagulieni jina la kazi" ameongeza Monalisa