Jumatatu , 26th Sep , 2022

Mkongwe wa mziki wa HipHop Mr II Sugu amepigia misumari kauli ya mapenzi yanaenda sawa na pesa kwa kushea ujumbe unaoeleza kuwa pesa haiwezi kununua mapenzi lakini ikiwepo inaleta raha.

Mr II Sugu na mke wake Happiness Mbilinyi

"Ni kweli money can't buy  love but mkwanja kiasi ukiwepo unaleta raha kwenye mapenzi. Dogo langu @fred_vunjabei atakubaliana na mimi" - Mr II Sugu 

Ikumbukwe hata Barakah The Prince alishaimba kwamba mapenzi sio pesa ila pesa ikikosekana mapenzi yanapungua.