"Mimi bado mdogo, nina miaka 19" - Anjella

Jumanne , 6th Apr , 2021

First Lady wa lebo ya Konde Gang Anjella amesema yeye bado ni mtoto mdogo sana ndio kwanza ana umri wa miaka 19 hivyo hataweza kuchanganya mapenzi na kazi kwa wakati mmoja kwani anahisi itamuharibia.

Msanii Anjella kutoka lebo ya Konde Gang

Anjella amesema kwa sasa yupo hayupo kwenye mahusiano kwa sababu wanaume wanahitaji uvumilivu pia yeye ni mtu wa dini hivyo anazingatia maadili  na hawezi kujihusisha na mapenzi.

"Ni kweli sina mpenzi na sipo kwenye mahusiano, kwanza mimi ni binti mdogo nina miaka 19 sitakiwi kujihusisha na hayo mambo siwezi ku-control mapenzi na kazi kwa wakati mmoja kwa hiyo itabidi nipige kazi na nilishaapa sitaki kuja kufa masikini hivyo lazima nipambane" amesema Anjella

Zaidi mtazame hapa chini kwenye video akizungumzia hilo.