Max Rioba akemea vibaya kuhusu neno la Connection

Jumatano , 23rd Sep , 2020

Meneja wa wasanii na mfanyabiashara Max Rioba amefunguka kusema matumizi mabaya ya internet yamefanya mpaka baadhi ya maneno kama 'connection' kuwa kwenye trend mbaya wakati kiuhalisia lina maana zuri.

Meneja wa wasanii Max Rioba

Akifunguka hilo kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio Max Rioba amesema Tanzania imepata fursa ya kutumia mitandao ya kijamii kwenye kujitangaza na biashara ila inatumika vibaya kwa kufanya mambo yasiyo na maana.

"Tumepewa fursa lakini tunaichezea, miaka 10 iliyopita hatukuwa na speed hii ya internet ila imekuja tunaitumia vibaya, ukitaja neno connection lipo kwenye trend mbaya sana wakati ni neno zuri tu, tunatumia internet kwa mambo yasiyo na maana".

Kingine kuhusu Max Rioba amefunguka kuacha kufanya kazi na aliyekuwa msanii wake Hamisa Mobetto kwa kusema walikuwa wamepishana kidogo na kila mtu amekuwa na mambo mengi.