Jumanne , 24th Nov , 2020

Hassan Sulaiman na Hussaini Dey ni mapacha wawili wa kiume wenye miaka 33, wameoa mapacha wenzao wa kike ambao wamefahamika kwa majina ya Hassana na Hussaina huko Kano Kaskazini mwa nchi ya Nigeria.

Mapacha wakiume walifunga ndoa na mapacha wenzao wa kike

Mmoja wa mapcha wa kiume Hassan Sulaiman amesema tangu walivyokuwa wadogo walikuwa wanasema kitu bora kwao ni kuoa mapacha wenzao ambapo wametimiza ndoto zao.

"Tangu tulipokuwa wadogo, tulikuwa tunafanya kila kitu pamoja, tulikuwa tunavaa nguo zinazofanana, kula chakula cha aina moja na tulisoma katika darasa moja, hata tulipoenda kusomea masuala ya afya namba ya usajili wa mtihani yake ilikuwa 010 wakati yangu ilikuwa 011

Aidha ameongeza kusema "Kwa muda mrefu tulipanga kuoa mapacha na hata familia yetu walituambia tuoe mapacha, kabla ya sasa, tumekuwa tukijaribu bahati yetu na sasa tuna furaha sana ndoto zetu zimetimia".

Chanzo : Opera News Nigeria , Daily Trust Nigeria, BBC Swahili.