Maneno ya Idris kuhusu video za Paulah wa Kajala

Jumatatu , 15th Feb , 2021

Mchekeshaji Idris Sultan ameshea 'comment' yake kuhusu sakata la video za mtoto wa staa wa filamu Kajala Masanja na Producer P-Funk Majani aitwaye Paulah Kajala, ambazo zinamuonesha akim-kiss msanii mmoja wa kiume wakiwa kwenye gari.

Mchekeshaji Idris Sultan

Katika sakata hilo Idris Sultan amesema haoni sababu ya mitandao ya kijamii ndiyo iwe ya kulaumiwa kwa asilimia 100 kama kuwa chanzo cha kuwaharibu watoto bali usimamizi wa wazazi na malezi.

"Sidhani kama 'social media' ndio ya kulaumiwa asilimia 100 kwa kuharibika kwa watoto siku hizi, kuna watoto wengi wanatumia hii mitandao na kwa usimamizi mzuri wa wazazi wao na wamefanya makubwa sana wengine hadi wamekuwa inspiration kwa watu wazima. turudi kwa wahenga mtoto umleavyo" ameeleza Idris Sultan 

Baada ya tukio hilo Kajala Masanja ameiomba Serikali na sheria kufuata mkondo wake kwani mtoto wake bado ni mwanafunzi na amedai msanii Hamisa Mobetto ndiyo amesababisha kwani alimchukua kwenda kula naye chakula cha mchana.