Alhamisi , 24th Sep , 2020

Staa wa kike kwenye muziki wa BongoFleva kwa sasa Nandy amenyoosha maelezo kuhusiana na madai ya kuwa na ujauzito wa Billnass baada ya kuonekana kula udongo kwenye mtandao wa Snapchat siku kadhaa zilizopita.

Wasanii na wapenzi Billnass na Nandy

Akizungumzia hilo mbele ya waandishi wa habari Nandy amesema watu wanamsema ni mjamzito kwa sababu ya ongezeko la mabadiliko yake ya mwili wake ambayo yanasababishwa na ukuaji.

"Watu wanasema mimi ni mjamzito kwa sababu ya mabadiliko ya mwili wangu ambayo yanasababisha  kukua haraka kama kunenepa, ukiangalia familia yetu wote wanamaumbo makubwa halafu ni wanene labda na mimi ndiyo nimefikia hatua ya kuwa hivyo" amesema Nandy 

Billnass na Nandy tayari wameshavalishana pete ya uchumba na kinachosuburiwa kwa hamu kubwa kwa sasa ni ndoa kati yao.