Jumanne , 20th Oct , 2020

Daktari Jimmy Minja amefunguka kusema hata Korodani zina uwezo wa kupata ugonjwa wa kuambukiza kama TB ambayo inaweza ukasabababisha ugumba kwa wanaume na kwenye upande wa uzalishaji wa mbegu za kizazi.

Daktari Jimmy Minja upande wa kulia wakati akifanyiwa mahojiano kwenye show ya DADAZ

Akizungumzia hilo kwenye kipindi cha DADAZ ya East Africa TV wakati anatoa sababu la tatizo la ugumba kwa wanawake na wanaume Daktari Jimmy Minja amesema kimila imezoeleka jukumu la kubeba ujauzito ni mwanamke, lakini kisayansi mama na baba wote wana uwezo sawa na asilimia 30 ya ugumba inaweza kuwa baba au mama, japo jamii nyingi inamsingizia mama. 

"Sababu za wanaume kuwa wagumba huwa tunasema ili mwanaume awe na uwezo wa kumpa ujauzito mwanamke awe na idadi sahihi na mbegu sahihi, kwa sababu unaweza ukatoa mbegu na zikawa hazitembei au ni ndogo, joto kwa wanaofanya kazi kwenye mionzi na viwandani

"Pia kuna maambukizi ya magonjwa kama TB, pia kuna TB ya korodani na saratani ya korodani, kwa hiyo vitu vyote hivyo vinaweza kusababisha mbegu zisiwe sahihi na magonjwa mengine kama kisukari" ameongeza 

Aidha kwa upande wa wanawake kuwa na tatizo la Ugumba ameeleza kuwa "Kwa wanawake mfumo mzima wa afya yake ya uzazi na hedhi unaanzia kichwani mwake kwenye ubongo ambapo kuna homoni za 'Pituitary na Hypothalamus' ambazo zina-control hedhi na mayai ya mwanamke pamoja na msongo wa mawazo