Jumatatu , 19th Jan , 2015

Ngoma mpya ya Madee, Vuvula imeibua mjadala katika moja ya mstari msanii huyo kuamua kumchana kiongozi wa kamati ya Miss Tanzania kama mtu asiyejielewa akimtaka kuwa makini kuhakikisha wakati ujao matatizo hayajitokezi tena.

Madee

Madee kwa maneno yake mwenyewe amesema kuwa, jina la kazi hii lina maana ya mtu ambaye hajielewi na mshamba na hapa anaufafanua mstari wake huu, sambamba na ushauri wa bure kwa vijana kuachana na matumizi ya dawa za kulevya.